Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amenusa ufisadi katika mradi wa
ujenzi wa nyumba za Avic ‘Avic Town’ na kuitaka taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuuchunguza mradi huo uliopo Kigamboni
jijini humo.makonda-new-jpg-ooHatua hiyo imefika baada ya kupata
malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo na kutolewa
pasipo kupewa fidia zao huku ekari 18 za Chama cha Mapinduzi
(CCM),zikichukuliwa kwa matumizi katika mradi huo.
Akizungumzia hatua hiyo,
Makonda amewataka watendaji wa serikali wanaohusika na taarifa za mradi
huo kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya dola kwani hataki kuona
wananchi wakidhulumiwa haki zao.“Sitaki kuona kigogo wala kijiti
anahusika katika mradi huo. Nitasimamia na polisi waliohusika katika
kuwatoa wananchi hawa waseme walitumia vigezo gani kuwatoa,”alisema.
Alisema wananchi
walioondolewa eneo hilo wafike kwa Mkuu wao wa Wilaya huku akiitaka
Takukuru kuchunguza mafaili ya mradi huo wa nyumba.
Akizungumza huku akilia
mkazi wa eneo hilo ambaye pia ni mwathirika wa mradi huo, Pascalina
Walioba alisema tangu mradi utambulishwe na kuanza kujengwa hawajalipwa
stahiki zao.
“Mimi ni mwathirika wa
mradi huo, tangu unaanzishwa na tukahamishwa kipindi hicho nilipaswa
kulipwa Sh 700,000 lakini hadi leo sijalipwa na thamani ya fedha
inaongezeka,”alisema na kisha kuangua kilio.
Mbunge wa Jimbo hilo,
Faustine Ndungulile alisema kuwa wapo watu walikuwa wakidai kuwa ujenzi
ule unahusisha nyumba za ulinzi wa usalama.
“Kuna hekari 18 za Chama cha Mapinduzi (CCM) zipo humo lakini tutalifualia,” alisisitiza Ndungulile.
Katika hatua nyingine
Wilaya hiyo imeahidiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), hadi
kufikia February mwakani watakuwana umeme wa uhakika.
Aidha wananchi wa eneo
hilo walitolewa hofu juu ya upatikanaji wa maji safi kwani tayari maji
yapo ya visima lakini hakuna mabomba ya kusafirisha maji hayo.
Akizungumzia mradi wa
maji katika mji huo, Mwakilishi kutoka Shirika la Maji saifi na Maji
taka(Dawasco),….alisema fedha zilizotengwa katika kusambaza maji katika
wilaya hiyo ni Sh bilioni 40 huku fedha zinazoitajika ili kukamilisha
mradi huo ni Sh bilioni 146.
No comments:
Post a Comment