Ilikuwa
kama mchezo wa kuigiza kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada
ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel
Mkumbo kufikishwa ili apandishwe kizimbani kujibu mashtaka sita,
likiwamo la kutishia kuua.
Tukio
zima la kumpeleka mahakamani, kumpandisha kizimbani na kumsomea
mashtaka kwa muda wa dakika 30 hivi lilitawaliwa na vituko. Kwanza, ni
jaribio la kuwaficha wanahabari.
Kabla
ya kufikishwa mahakamani, Polisi mkoani Morogoro iliwaarifu wanahabari
kuwa ingetoa taarifa kuhusu mkurugenzi huyo lakini saa 4:30 asubuhi
wakati Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro,
Ulrich Matei akijiandaa kuzungumza nao, alipigiwa simu akatoka nje ya
ukumbi na aliporejea alisema hawezi kutoa taarifa tena na akaondoka.
Waandishi
walipofika mahakamani saa 5:00 asubuhi walikuta Kamanda Matei akishuka
kwenye gari na alipanda tena akasogea kando kuzungumza na baadhi ya
askari wake.
Pili,
baada ya hakimu kumaliza kusikiliza kesi hiyo, Mkumbo hakurudishwa
mahabusu mahakamani hapo kama ilivyo ada ili kusubiri utaratibu mwingine
badala yake mshtakiwa huyo alihamishiwa chumba cha hakimu ambacho
hakikuwa na kesi inayoendelea.
Humo
ndugu zake walimpelekea koti kubwa jeusi na kofia aina ya pama, hivyo
alitoka akiwa tofauti na alivyoingia akiwa na fulana yenye rangi nyeupe,
bluu na nyeusi. Baada ya kuvaa alitoka akiwa amezingirwa na polisi,
huku ndugu wakiwazuia wanahabari kumpiga picha.
Mashtaka dhidi yake
Mkumbo
ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam alipandishwa kizimbani
kujibu mashtaka sita, la kwanza likiwa la kutishia kuua kwa bastola na
la pili ni la usalama barabarani lenye makosa matano.
Alisomewa
mashtaka hayo na mawakili wa Serikali Sunday Hyera na Edgar Bantulaki.
Katika shtaka la kwanza, mbele ya hakimu Agripina Kimaze anadaiwa Oktoba
15, saa 10:30 jioni alitenda kosa la kutishia kuua eneo la Mkambarani,
Manispaa ya Morogoro.
Anadaiwa
katika shtaka hilo la jinai namba 226 la mwaka 2016, alitishia kumuua
kwa bastola askari namba 5057, Koplo Tuti Ndaga wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Mkoa wa Morogoro, kinyume na kifungu namba 89 (1),(2),(a) cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16.
Katika shtaka la pili la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani lenye makosa matano, ilidaiwa kuwa; kwanza, siku na muda huo eneo la Mbuyuni Mkambalani, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado lenye rangi ya kijivu bila kuwa na leseni.
Katika shtaka la pili la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani lenye makosa matano, ilidaiwa kuwa; kwanza, siku na muda huo eneo la Mbuyuni Mkambalani, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado lenye rangi ya kijivu bila kuwa na leseni.
Pili,
ilidaiwa alikuwa akiendesha gari hilo ambalo halikuwa na bima; tatu,
alikutwa akiendesha kwa mwendo kasi; na nne, alikataa kupeleka gari
Kituo cha Polisi cha Kingoluwira kama alivyoamriwa na askari, WP namba
5392 Sajenti Anna.
Ilidaiwa
katika shtaka la tano kwamba, wakati akiendesha alisimamisha gari
katikati ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam kwa uzembe, bila
uangalifu wala kuzingatia watumiaji wengine wa barabara. Mkurugenzi huyo
alikana mashtaka yote yanayomkabili.
Hakimu
Kimaze alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kwamba awe na mdhamini
mmoja kwa kila shtaka, yaani shtaka la jinai na la usalama barabarani
lenye makosa matano, wote wawe wakazi wa Morogoro na mmoja akitakiwa
kuweka dhamana ya Sh500,000 kwa kosa la kwanza na Sh1 milioni kwa kosa
la pili.
Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huru, huku gari likiendelea kushikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro.
Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huru, huku gari likiendelea kushikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro.
Hakimu
Kimaze aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31, usikilizwaji wa awali
utakapoanza baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi umekamilika.
No comments:
Post a Comment