Chama
cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa siku 15 kwa Serikali kumaliza madai
yao ya muda mrefu vinginevyo watachukua maamuzi magumu.
Rais
wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa uvumilivu wao umeelekea kufikia
ukingoni kwani wamekuwa wakikaa mezani na Serikali mara kwa mara na
kupewa ahadi za kutatua matatizo yao lakini hadi sasa hazijatekelezwa.
Alisema
kuwa Agosti 22 na 23 mwaka huu, Baraza la chama hicho cha walimu
lilipitisha maazimio kupitia kikao chake, maazimio ambayo yalisainiwa
pia na upande wa Serikali kwa ahadi kuwa wangeyafanyia kazi lakini
imeendelea kuwa kimya.
“Siku
chache baadae tuliambiwa tusubiri mchakato wa kuhakiki watumishi
ukamilike. Lakini licha ya mchakato huo kukamilika Serikali imeendelea
kukaa Kimya,” Mukoba anakaririwa na Tanzania Daima.
Aliyataja
madai hayo kuwa ni pamoja na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule,
muundo wa madaraka, walimu kutopandishwa madaraja na kulipa madeni ya
walimu.
“Ninachoweza
kukwambia ni kwamba mwishoni mwa Oktoba ambao umebakiza siku 15
tutachukua uamuzi mzito ambao haujawahi kutokea na hatutaki lawakama
kutoka sehemu yoyote ile,” alisema Mukoba.
No comments:
Post a Comment