Mahakama
kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika
jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa bilcanas.
Hukumu
hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa
Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu
katika jengo hilo.
Amesema
katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana
na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa
Mbowe HotelS.
Wakili
wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe
hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi
kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.
Nae
Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na
kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata
wanaweza kuamua katika kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment