Baada ya
kurejea kwa safari za ndege nchini Kenya, Serikali ya nchi hiyo jana
October 17, 2016 asubuhi ilikutana na chama cha marubani wa ndege za
Kenya Airways na usimamizi wake ili kuweza kutatua mzozo ulioibuka kati
ya muajiri ambaye ni Serikali ya Kenya na marubani wake.
Ikumbukwe mkutano huo umeitishwa siku moja kabla ya mgomo, ambao ulipangwa kufanyika October 18, 2016.
Ijumaa ya
wiki iliyopita, Waziri wa ajira nchini Kenya, Phyllis Kandie alituma
barua kwa pande zote mbili, pamoja na kuteua kamati ya wajumbe watano
kushughulikua mgogoro huo.
Chama cha
wafanyakazi nchini Kenya KALPA kimetoa mapendekezo yake ambapo moja ya
walichoagiza ni pamoja na kutaka Mkurungenzi Mtendaji wa shirika la
ndege Kenya Airways, Mbuvi Ngunze na mwenyekiti Dennis Awito wajiuzulu
nafasi zao mara moja.
Serikali
ya Kenya imeona madhara ya mgomo uliopangwa kufanywa na Marubani wa
shirika la ndege la Kenya Airways, baada ya abiria kukata tiketi za
safari zao na kucheleweshwa kwa safari za ndege mwezi uliopita.
October
16, 2016, Kenya Airways ililazimika kukatisha safari zake tano katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya marubani na
wafanyakazi wa shirika hilo kugoma kufika uwanjani.
No comments:
Post a Comment