Thursday, 13 October 2016

WATU WATANO WAKIWEMO WACHINA WAWILI WAMEKAMATWA MKOANI MTWARA WAKIBADILI TAREHE ZA MATUMIZI YA DAWA


Watu watano wakiwemo raia wawili wa China na Watanzania watatu wamekamatwa Mtwara kwa kutuhumiwa kubadili tarehe zilizokwisha muda wa matumizi kwenye dawa za kilimo (expire date) ili dawa hizo ziingizwe tena sokoni na kuonekana bado zinafaa kwa matumizi.

Inadaiwa watuhumiwa hawa wamefanikiwa kubadilisha dawa hizo kwenye mabox zaidi ya mia sita ( 600) na kuzifanya zionekane mpya ambapo Kamanda wa Polisi Mtwara amesema Watuhumiwa hao walikamatiwa Nangwanda.

Makachero wa Polisi baada ya kupewa taarifa waliwahi kwenye eneo la tukio na kukuta watu wanne wakikwangua chupa kuondoa nembo iliyoonyesha dawa hiyo ilitengenezwa tarehe 28 February 2013 na muda wake wa matumizi umekwisha tarehe 27 February 2016.

Nembo mpya feki waliyoitengeneza Wachina hawa inasomeka dawa imetengenezwa tarehe 20 February 2016 na inamaliza muda wa matumizi tarehe 19 February 2019

No comments:

Post a Comment