Serikali
imesema imetenga jumla ya shilingi bilioni 70 kwa ajili ya kununua dawa
na vifaa tiba ili kumaliza tatizo la ukosefu wa dawa nchini.
Aidha imetenga jumla ya shilingi bilioni 85 kwa ajili ya kupunguza deni linalodaiwa na bohari ya dawa MSD lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya zenye ubora.
Akifungua
mkutano mkuu wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini jana mjini
Dodoma makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassan alisema dawa hizo
zitakazonunuliwa zitaenda moja kwa moja katika vituo vya afya vilivyopo
hapa Nchini.
Alisema
lengo la serikali ni kupunguza changamoto zilizopo katika sekta ya afya
huku akiweka bayana dhamira ya serikali ya kujenga kiwanda cha Dawa
katika mkoa wa Simiyu.
Mbali
na hilo alizungumzia suala la tiba asili na tiba mbadala na kuitaka
Wizara ya Afya maendeleo ya jamii,jinsia,Wazee na Watoto kuhakikisha
wanazipa umuhimu kwa kuzitambua na kuzisajili.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Waganga hao dokta Sudi Leonard aliiomba
serikali kutatua tatizo la dawa na vifaa tiba lililopo nchini ambalo
limekuwa likisababisha malalamiko na manung`uniko kwa wananchi hasa kwa
makundi maalum kama wajawazito,watoto,wazee na wenye magonjwa sugu.
Mkutano
huo ni wa siku nne wenye lengo la kujadili kwa pamoja masuala
mbalimbali yahususyo afya na ustawi wa jamii,kubadilishana uzoefu na
kujadili namna ya kutatua changamoto zilizopo ukibeba kauli mbiu isemayo
mfumo na huduma bora za afya ni nguzo muhimu kuelekea Tanzania yenye
viwanda na uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment