Serikali
imesitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude
Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo
utaratibu mwingine utakapotolewa.
Mpango
huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa
Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka
magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo
ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo.
Alisema
wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao. Mrema
alisema jana kuwa mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na
kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa.
No comments:
Post a Comment