Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha
zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na
masomo zinapelekwa vyuoni ifikapo leo.
Agizo
hilo lilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wabunge mbalimbali kuomba
miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo
kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Mwongozo
kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete
aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo.
Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga aliitaka Serikali kutoa maelezo.
Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga aliitaka Serikali kutoa maelezo.
Akitoa
kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako alisema fedha za mikopo kwa ajili
ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita.
“Tatizo
lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza
fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na
waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”alisema.
Kuhusu
wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wote
wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama
ilivyokuwa mwaka uliopita.
Alisema
wanafunzi ambao vyuo vyao vimewasilisha HELSB taarifa za matokeo, Bodi
imekwishawatumia fedha vyuoni kwa ajili ya kuwapa mikopo wanafunzi hao.
Hata
hivyo, alisema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea
na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo.
Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni.
“Wizara
yangu imekwishaagiza vyuo vyote ambavyo havijawasilisha matokeo ya
mitihani ya wanafunzi wao kwa mwaka wa masomo uliopita, kufanya hivyo
mara moja,”alisema.
Ndalichako
alisema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni
zilikwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na
wanaoendelea na masomo.
Akizungumzia
utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17, Ndalichako alisema katika
mwaka huo, Sh483 bilioni zimetengwa na zimelenga kutoa mikopo kwa
wanafunzi 119,012, wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo na wa mwaka
wa kwanza 25,717.
Ndalichako
alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 wanafunzi 58,010 walidahiliwa na
Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na orodha yao iliwasilishwa HELSB na hadi
Novemba 2, mwaka huu, wanafunzi 21,190 wa mwaka wa kwanza wamepewa
fedha. Kati yao 4,321 ni yatima, 118 wenye ulemavu na 87 ni waliosoma
sekondari kwa ufadhili wa taasisi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment