Monday, 17 October 2016

YANGA VS AZAM NANI ZAIDI??

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea jana Jumapili ya October 16 2016 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Dar es Salaam Young Africans walikuwa wageni wa Azam FC katika mchezo huo wa nane kwa Yanga wa tisa kwa Azam FC.
Mchezo huo wa Yanga na Azam ulianza kwa wenyeji Azam FC kuingia uwanjani na kumbukumbu ya kufungwa  goli 1-0 mchezo uliopita dhidi ya Stand United, wakati Yanga walikuwa na kumbukumbu ya ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru.
Rekodi za ushindi zilizopita za Yanga hazikuifanya Yanga ipate matokeo na Azam kukubali kufungwa mchezo uliopita, haikufanya wawe dhaifu mbele ya Azam FC na kufanya mchezo umalizike kwa suluhu 0-0, matokeo hayo yanaifanya Azam FC iendelee kuzurura nafasi ya 7

No comments:

Post a Comment