Baadhi
ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kichama wakiongozwa na Rais Dkt
John Pombe Magufuli (wa tano kulia) wakiwa katika viwanja vya Karimjee
mapema leo asubuhi kutoa heshima ya mwisho na kuaga mwili wa Marehemu
Dkt Didas Masaburi,aliyefariki wiki iliopita katika hospitali ya Taifa
ya Muhimbili,wakishiriki
***
Rais
John Magufuli leo ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam
kuuga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi
aliyefariki Jumatano iliyopita na kusema Masaburi ana wake wanne au
watano na watoto zaidi ya 20.
Kauli
ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk
Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet
Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa
waombolezaji.
Alipopewa nafasi ya kuzungumza Dk Magufuli alisema anamfahamu Dk Masaburi kuwa alikuwa na wake wanne au watano hivi.
Alisema hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20.Rais Magufuli alisema Masaburi alikuwa rafiki yake,ndugu yake na mpiganaji mwenzake ndani ya CCM.
Baadhi ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa mpendwa wao Dkt Didas Masaburi
No comments:
Post a Comment