Serikali
kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia
Desemba mwaka huu mpaka Januari 2017 itaanza kutoa namba maalum za
utambuzi kwa wananchi.
Mkakati
huo umetangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la
kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.
Alisema
tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35
zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi
wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa
zinazowahusu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la
awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua
watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.
No comments:
Post a Comment