Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa ya mkoani Geita, Dennis Otieno
anadaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM
kwenye mahafali ya kidato cha nne.
Pia,
taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya
walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu
ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta
michango yote mashuleni.
Otieno,
ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo
kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti
wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye
amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya
Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment