Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli, Janeth, amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Jana Ikulu imetoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji.
Taarifa ya ikulu ilisema , alipokuwa anamjulia hali mkewe, pamoja na balozi na waziri mstaafu wa Tanzania Omar Ramadhan Mapuri, wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji walimshukuru kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili
Pia walisema kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na
mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa
matibabu jana Novemba 10, 2016. Kulia ni Dkt Edward Ngwale akiwa na
wauguzi katika wodi hiyo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia
hali Waziri wa Zamani Balozi Omar Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa
kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
Dar es salaam akipatiwa matibabu jana Novemba 10, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na
wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye
anapatiwa matibabu jana Novemba 10, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji
baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa
ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na
mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo jana Novemba 10, 2016.
No comments:
Post a Comment