Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) Bw.Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali imeanza Ujenzi wa reli ya kati,ujenzi wa kiwango cha Standard Gauge yenye upana wa Mita 1.345.
Akizungumza jana Jijini Dar es salaam na Waandishi wa Habari,Kadogosa alisema
kuwa ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kwanza katika nchi ya Tanzania hasa
baada ya Uhuru utapelekea kuleta na kuhamasisha maendeleo kwa haraka
katika sekta ya Kilimo,biashara,Madini na viwanda.
Hata Hivyo Mkurugenzi huyo alisema
kukamilika kwa mradi wa Reli ya kati utaleta manufaa mengi ya kiuchumi
na ya kijamii na kusaidia kuboresha pamoja na kuunganisha usafirishaji
kwa nchi zisizokuwa na bandari kuelekea masoko ya Afrika na Dunia kwa
ujumla.
"Kukamilika
kwa Reli ya kati Utavutia uwekezaji katika maeneo ambayo mfumo huo wa
Reli utapita na utaboresha usafirishaji,lakini pia utachochea maendeleo
ya shughuli za Madini na usafirishaji wa nidhaa nje ya nchi, utasaidia
kuokoa barabara zetu na kupunguza gharama kubwa ya ukarabati wa
barabara,"alisema Kadogosa.
Pia aliongeza
kuwa miradi hii imekuwa ikigharamiwa na Serikali ilikutimiza azma yake
kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa ajili ya jamii ya watanzania hasa
tunapoelekea katika uchumi wa viwanda kupitia sekta ya usafirishaji.
No comments:
Post a Comment