Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuagiza Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kortini, mbunge huyo amedai hana taarifa hizo hivyo hawezi kujisalimisha popote.
Lissu
ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, alidai
atajisalimisha tu kwenye vyombo vya dola au kwenda mahakamni ikiwa
atapelekewa barua aliyoandikiwa na mahakama na kutiwa saini na kugongwa
muhuri na hakimu.
“Kaka,
mimi siwezi kufanyia kazi za magazeti katika masuala ya kisheria, nipo
hapa ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kama mnavyoniona niko
katika kuwawakilisha wananchi wa jimbo langu,” alieleza Lissu.
Mwanasheria
huyo mkuu wa Chadema alitoa maelezo hayo jana alipohojiwa kuhusiana na
habari zilizoandikwa na vyombo vya habari, kwamba Mahakama ya Kisutu
juzi iliagiza mbunge huyo akamatwe baada ya kushindwa kuhudhuria katika
kesi inayomkabili.
Mbali
ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Lissu, pia iliagiza
iandaliwe hati ya kuitwa mahakamani kwa wadhamini wake ili wajieleze kwa
nini wasilipe fungu la dhamana walilotia saini ambalo ni Sh10 milioni.
Kwa
mujibu wa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Thomas Simba, Lissu amekuwa hahudhuri
kortini kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na wahariri wa
gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti,
Ismail Mehboob.
Katika
kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu, Dar es
Salaam, Lissu na wenzake walikula njama za kuchapisha chapisho la
uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari: “Machafuko
yaja Zanzibar”.
Juzi,
siku ambayo kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena, Lissu hakuwapo mahakamani
kutokana na kile mdhamini wake Robert Katula alichodai kuwa mshtakiwa
huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza
hivyo asingeweza kuhudhuria.
Kutokana
na maelezo hayo wakili wa upande wa Jamhuri, Patrick Mwita aliomba
mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa jambo ambalo Hakimu
Simba alikubali pamoja na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba
21, mwaka huu.
Alipoulizwa
kuhusu hatua hiyo, Lissu alisema kuwa wito wa kwenda mahakamani ni
lazima barua iwe imeandikwa na kugongwa muhuri na kutiwa saini ya hakimu
wa mahakama na siyo kusikia na kwenda bila ya kuwepo kwa wito kamili.
No comments:
Post a Comment