Serikali
ya Israel imeanza kutoa huduma za viza moja kwa moja kutokea jijini Dar
es Salaam ambapo kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa
Jumanne Maghembe, hatua hiyo itachochea ukuaji wa biashara pamoja na
ushirikiano wa kidiplomasia.
Awali,
viza zilikuwa zikitolewa jijini Nairobi nchini Kenya lakini hivi sasa
huduma hiyo itakuwa ikipatikana jijini Dar es Salaam ambapo Waziri
Maghembe ametaja baadhi ya faida chache za utolewaji wa huduma hizo hapa
nchini kuwa ni kupungua kwa urasimu na gharama za kutafuta viza, kukua
kwa ushirikiano katika nyanja zote za uchumi, elimu ulinzi pamoja na
usalama.
Balozi
wa Israel nchini Kenya Bw. Yahel Vilan amesema hatua hiyo itakuza
uhusiano wa kidiplomasia hususani kwenye eneo la uchumi, kutokana na
uzoefu mkubwa iliyonao taifa hilo ambalo hivi sasa limepiga hatua kubwa
kwenye uchumi na teknolojia.
Kwa
upande wake, Bi. Pooja Lalji amesema wamejipanga kuhakikisha
wafanyabiashara wanaokwenda Israel wanapata viza zao mapema na hivyo
kuchochea biashara baina ya Tanzania na taifa hilo la Mashariki ya Kati.
No comments:
Post a Comment