POLISI
mkoani Dodoma inawashikilia walimu watatu wa shule za sekondari kwa
tuhuma ya kuwazuia wanafunzi wa kidato cha nne, kufanya Mtihani wa
Taifa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kwamba walimu hao wa
shule za sekondari za Zoissa na Mnyakongo wilayani Kongwa, walikamatwa
Novemba Mosi mwaka huu.
Kamanda
Mambosasa alisema kwamba, wakati wa mtihani wa somo la Kiingereza,
walimu hao walimzuia mwanafunzi Amina Said wa shule ya sekondari Zoissa
kwa madai ya kuwa ni mjamzito na kumpeleka kituo cha afya, kupimwa muda
wa mtihani, lakini majibu yalionesha hakuwa na ujauzito.
Aidha,
mwanafunzi Bahati Ntigonza wa shule ya sekondari Mnyakongo, alizuiliwa
kuingia katika chumba cha mtihani kwa kuwa hakuvaa sare ya viatu, hivyo
alirudishwa nyumbani kuvaa viatu huku wenzake wakiendelea na mtihani.
Kamanda
Mambosasa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Lukonge Mwezo
ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mnyakongo, Omari Athumani Mkuu wa
Shule ya Sekondari Zoissa na Daud Suleimani John aliyekuwa mwalimu wa
zamu katika shule ya sekondari Mnyakongo.
No comments:
Post a Comment