Tarehe
Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu sana kwa watanzania na Mimi
binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa mgombea wa upinzani.
Naamini
nilileta sura na msisimko mpya katika siasa za Tanzania.Nilishirikiana
na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana yake ni nini.
Napogeuka
nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja kubwa sana hasa kwa jinsi
watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini makubwa
kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina
wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.
Chini
ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha kampeni za kiungwana kama
tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka visiwani ambako Maalim
Seif aliporwa dhahiri ushindi.
Kwa
mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi, tulishindwa uchaguzi
ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha mwagika ambayo
hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini tunataka
mabadiliko,hivi sasa kila mtu anakiona.
Pamoja
na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo lakini maisha yamezidi
kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka,Elimu bure
iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa kaa la
moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani
madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.
Nawashukuru
sana wananchi kwa imani kubwa waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa
ujumla.Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwengine,
kwahiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza.Kasi,nguvu, ari na hamasa
niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.
No comments:
Post a Comment