Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar umeingia kwenye jaribio jingine, baada ya
Wazanzibari 40,000 kufungua kesi mahakamani kupinga uhalali wake.
Kesi
hiyo ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki
(EACJ) na Rashid Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999, katika Masijala
ndogo ya mahakama hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.
Wadaiwa
katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Adiy anasema kuwa msingi wa kesi hiyo ni kwamba Muungano huo haukuanzishwa kisheria.
“Sisi
tunadai Muungano huu hauko kwa misingi ya kisheria na kutokana na
ushahidi tulionao, uko kisiasa tu na jambo hili linahitaji mfumo na
mwenendo wa kisheria kwa kuwa wenye mamlaka ya nchi ni wananchi,” alisema Adiy.
Alisema
kutokana na nyaraka walizonazo wanapinga hati ya Muungano inayodaiwa
ilisainiwa Aprili 22, 1964 na wanapinga uamuzi wa Baraza la Mapinduzi
kuridhia Muungano huo.
Wanapinga barua ya Mei 6, 1964, iliyopelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), kuelezea kutambuliwa kwa Muungano huo.
Pia,
wanapinga uhalali wa barua ya Novemba 2, 1964 iliyopelekwa UN ikielezea
matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria
iliyopitishwa na Bunge Desemba 10, 1964 ikielezea matumizi ya jina la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Adiy
na wenzake wanadai kwa kuwa Muungano ni wa kisiasa, ndiyo maana hauwezi
kuleta manufaa kwa pande zote mbili hususani uwiano wa kiuchumi na
kielimu.
Baada
ya kuwasilisha nyaraka zao wanasubiri kesi hiyo isajiliwe kwa kupewa
namba katika Mahakama hiyo na kupangiwa taratibu za usikilizwaji wake.
Mbali
na Wazanzibari 40,000, pia alisema wanayo majina mengine ambayo
watayawasilisha mahakamani baadaye, kesi itakapokuwa imeanza
No comments:
Post a Comment