Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mjadala
ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoonekana kwenye misiba
ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu wa zamani,
Joseph Mungai.
Sitta
alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda
kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki Mungai.
Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa.
“Mdogo
wangu Bahati Lowassa ni ofisa ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa
anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku zote nilikuwa huko kumuangalia.
Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,” Lowassa
Mwanasiasa
huyo ameongeza kuwa alikuwa pamoja na waombolezaji kwa kutuma salamu
zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia vyombo vya habari pamoja
na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa
familia ya Mungai.
No comments:
Post a Comment