Leo
na mimi nipaze sauti yangu imfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa Mafanikio Makubwa aliyoyapata ktk
kipindi cha Mwaka mmoja wa utawala wake tangu aingie madarakani mnano
Novemba 05, 2015.
Rais
Magufuli kwa kiasi kikubwa amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma.
Leo ofisi nyingi za utumishi wa umma zina nidhamu ya hali ya juu sana,
watu wanatambua vizuri nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya
ktk Utumishi wao. Huduma zenye kukidhi matakwa ya wananchi zimerejea.
Rais
Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti matumizi ya fedha za
Serikali kwa kuzuia na kufuta matumizi yasiyokuwa ya lazima kama safari
za nje ambapo ktk kila safari kwa sasa ni lazima Ikulu ibariki kwa
kutoa Kibali na kuruhusu idadi ndogo tu ya watu na mara nyingine
mabalozi kuiwakilisha Tanzania, kuondoa posho zisizo za lazima n.k
Rais
Magufuli alielekeza fedha mbalimbali ambazo zilitengwa kwa matumizi
Maalum Mfano Fedha kwa ajili ya Semina kwa Baraza la Mawaziri, Fedha kwa
ajili Sherehe ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Uhuru - 09 Desemba 2015 n.k
Mh. Rais alielekeza zikafanye Shughuli za Kimaendeleo ikiwemo kununua
Vitanda vya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutengeneza Madawati kwa
ajili ya Shule za msingi ili kuboresha Elimu.
Rais
Magufuli alituahidi endapo atachaguliwa Elimu ya msingi na Sekondari
itakuwa ni BURE ambapo ametimiza sasa Elimu kwa Shule za Msingi na
Sekondari ni BURE kabisa.
Rais
Magufuli aliahidi atafufua Shirika la Serikali la Ndege la ATCL kwa
kununua Ndege Mpya ambapo tayari Mheshimiwa Rais ametimiza Ahadi yake
kwa Kununua Ndege Mbili Mpya na leo ameahidi kutuletea Ndege Kubwa aina
ya Boeing yenye uwezo wa Kubeba abiria zaidi ya 240 ili kukuza uchumi
wa Nchi kupitia Sekta ya Utalii.
Rais
Magufuli amefanikiwa kusimamia ipasavyo Ukusanyaji wa Mapato ya
serikali na Kudhibiti Matumizi yake. Hongera pia Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais ktk hili.
Rais
Magufuli alituahidi kupambana na Ufisadi na Kuendeleza Vita dhidi ya
Wala Rushwa kwa Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Ufisadi na Rushwa na
tayari mahakama ya Kushughulikia Ufisadi & Rushwa inaishi na leo
naamini imesikiliza Kesi moja.
Rais
Magufuli ameendelea kuboresha barabara kwa Kukijenga kwa Kiwango cha
lami mfano kama ile ya Mwenge Dar es Salaam & Mwanza.
Mheshimiwa
Rais aliahidi kuhamishia Serikali yake Makao Makuu ya Tanzania Mjini
Dodoma na tayari amekwisha anza kutekeleza kwa kuhamisha Ofisi ya Waziri
Mkuu na Wizara mbalimbali.
Rais
Magufuli aliahidi kukuza Uchumi wa Nchi yetu kwa kuifanya Tanzania ya
Viwanda na wote tumeshuhudia Juhudi za Mheshimiwa Rais za Kutafuta
wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili yawekeze nchini.
Ndugu
zangu yako Mengi sana aliyofanya Rais Magufuli mwenye macho haambiwi
tazama ila naomba niishie hapo. Ijapokuwa Bado Changamoto ni nyingi na
watu wataona Maisha yamekuwa magumu lakini tutambue na kuelewa hali hiyo
haina budi kuja kwani Nchi iko katika kipindi cha Mabadiriko ya
kiuchumi kitaalamu tunaita " TRANSITION PERIOD " ambapo kutokana na
Juhudi za Mheshimiwa Rais kuujenga uchumi wa Nchi yetu ni lazima
mwanzoni tutaona Mabadiriko fulani fulani hivyo Watanzania wenzangu
tuvute subira kwa maisha Mazuri yaja. Tumpe nafasi Mh. Rais apambane kwa
ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu na sisi kwa nafasi zetu tumpe
ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa Bidii sana.
Ama
Kwa Hakika Rais wetu anastahili pongezi nyingi sana na Mimi Robert PJN
Kaseko Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha nichukue nafasi hii
kukupongeza Rais wangu na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Mh. DKT. John Pombe
Magufuli kwa kutuletea Maendeleo makubwa na Mabadiriko ya kweli kwa
kipindi cha Mwaka mmoja tunashirikiana toka tukuchague utuongoze,
Mabadiriko ambayo kiukweli sisi Wananchi wa Tanzania tulisubiri kwa
Muda mrefu sana na nizidi kukutia moyo Mh. Rais usirudi nyuma endelea
mbele tunatambua vikwazo ni vingi na Kazi ni ngumu lakini namuomba
Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu, akupe afya njema na ulinzi wake ili
uendelee vyema kuwaletea Maendeleo Wananchi wako maana wewe ni Mchapa
Kazi Kwelikweli tunakufahamu vizuri. HAPA KAZI TU. CCM Hoyeeeeeee.
Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
November 04, 2016.
No comments:
Post a Comment