Monday, 26 March 2018
Tuesday, 22 November 2016
Waliohamishiwa UDOM kutoka St Joseph kurudia mwaka
Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Imewataka wanafunzi wa St. Joseph
walioamishiwa katika chuo kikuu cha Dodoma kurudia mwaka kwa kile
kilichobainika kuwa na ujuzi na maarifa usiokidhi viwango vya chuo cha
Dodoma.
Wizara hiyo pia imesema kwamba watakaogomea uamuzi huo watatakiwa kurudi makwao .
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Joyce Ndalichako alisema, ni lazima wanafunzi hao warudie mwaka
kwani wamepimwa na kubainika kuwa na uwezo mdogo hivyo hatua ya kuwataka
kurudia mwaka ni nafasi ya pili kwao.
Prof.
Ndalichako alisema, kwa sasa wizara yake inaandaa ripoti ya vyuo
vinavyofundisha chini ya viwango ambapo amesema mara tu baada ya
kukamilika ripoti hiyo, itatolewa na kwamba kwa wale wanafunzi ambao
vyuo vyao vimefungwa kwa kutokidhi vigezo ni lazima wapimwe kiubora ili
kupata wanafunzi watakao kidhi vigezo vya soko la ajira.
Aidha,
Prof. Ndalichako ametoa onyo kwa wanafunzi ambao wamegushi nyaraka
mbalimbali ikiwemo za vifo vya wazazi wao ama ugonjwa na kufanikiwa
kupata mkopo wa elimu ya juu kwa njia ya udanganyifu kuwa wizara hiyo
inafanya uhakiki na pindi watakapo bainika hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao.
Godbless Lema Kujaribu Tena Bahati yake Leo Mahakamani baada ya Kusota Mahabusu kwa Siku 19
Jaribio
jingine la maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),
Godbless Lema linafanyika leo baada ya kusota mahabusu tangu akamatwe
mkoani Dodoma Novemba 3.
Lema
anayekabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John
Magufuli, ombi hilo la dhamana linakuwa la tatu baada ya kukwama mara
mbili tangu alipoingizwa mahabusu.
Lema
ambaye anatetewa na mawakili sita; Peter Kibatala, John Mallya, Charles
Adiel, Adam Jabir, Faraja Mangula na Sheck Mfinanga, dhamana yake licha
ya kutolewa na Hakimu Mkazi, Desdery Kamugisha ilipingwa kutokana na
notisi ya rufani iliyowasilishwa na mawakili wa Serikali.
Baada
ya notisi hiyo, Lema aliandika barua Mahakama Kuu kuomba mapitio ya
kesi hiyo kwa maelezo kuwa taratibu za kisheria zilikiukwa kutokana na
hakimu kutoa dhamana lakini akashindwa kukamilisha masharti ya dhamana
na kupokea hoja za Jamhuri.
Hata
hivyo, wakili mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha
pingamizi jingine kupinga Mahakama Kuu kufanya marejeo ya kesi hiyo.
Kadushi
aliwasilisha hoja mbili za kisheria juu ya kuweka pingamizi la ombi la
mbunge huyo kuwa muombaji hakukidhi vigezo vya kuiomba mahakama irejee
maamuzi ya mahakama kwa kuwa badala ya kuiandikia mahakama barua ya
kuomba ifanye mapitio ya maamuzi hayo, angetakiwa akate rufaa juu ya
maamuzi ya mahakama.
Monday, 21 November 2016
MAKONDA AITAKA TAKUKURU KUCHUNGUZA MADAI YA UFISADI MRADI WA AVIC TOWN
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amenusa ufisadi katika mradi wa
ujenzi wa nyumba za Avic ‘Avic Town’ na kuitaka taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuuchunguza mradi huo uliopo Kigamboni
jijini humo.makonda-new-jpg-ooHatua hiyo imefika baada ya kupata
malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo na kutolewa
pasipo kupewa fidia zao huku ekari 18 za Chama cha Mapinduzi
(CCM),zikichukuliwa kwa matumizi katika mradi huo.
Akizungumzia hatua hiyo,
Makonda amewataka watendaji wa serikali wanaohusika na taarifa za mradi
huo kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya dola kwani hataki kuona
wananchi wakidhulumiwa haki zao.“Sitaki kuona kigogo wala kijiti
anahusika katika mradi huo.
Rais Magufuli ateua Naibu Kamishna Mkuu wa TRA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana
tarehe 20 Novemba, 2016 amemteua Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Bw. Charles E. Kichere anajaza nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA iliyokuwa wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Uteuzi huu umeanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Friday, 18 November 2016
Mamlaka ya Bandari Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti
mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika
Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth
Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza
kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo.
Alisema ujio wa
boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande
wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa
mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi.
Godbless Lema Akwama Tena Kupata Dhamana.......Arudishwa Gereza la Kisongo, Hatima Yake Kujulikana Wiki Ijayo
Hatma
ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema),
ilishindwa kujulikana jana baada ya mawakili wa Serikali kuweka
pingamizi, wakipinga Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kusikiliza maombi ya
dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa mshtakiwa.
Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jaji Sekela Moshi, alisema kutokana
na pingamizi hiyo, atasikiliza hoja za sheria zilizowasilishwa
mahakamani hapo kabla hajatoa uamuzi wowote juu ya dhamana ya mshtakiwa.
Aliwaelekeza mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za sheria kabla mahakama haijaendelea na hatua yoyote.
Jaji Moshi alisema atatoa uamuzi kuhusu mvutano huo wa sheria, Novemba 22, mwaka huu
Wakuu 7 wa Mikoa Hatarini Kutumbuliwa kwa Kushindwa Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli
Wakuu wa mikoa saba wako hatarini kutumbuliwa kutokana na kushindwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati katika mikoa yao.
Akizungumza
jana alipokuwa akipokea madawati 3,500 yenye thamani ya milioni 300
kutoka benki ya NMB, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George
Simbachawene alisema mikoa ya wakuu hao saba inaoongoza kwa upungufu wa
madawati.
Aliwataja kuwa ni wa Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma.
Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli.
Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli.
Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro, amesema kama Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika
operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua zaidi kwa
sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
Usalama Mkoani Dar es salaam.
Thursday, 17 November 2016
NIDA kuanza kutoa namba za utambulisho Desemba
Serikali
kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia
Desemba mwaka huu mpaka Januari 2017 itaanza kutoa namba maalum za
utambuzi kwa wananchi.
Mkakati
huo umetangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu
Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la
kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.
Alisema
tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35
zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi
wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa
zinazowahusu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la
awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua
watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.
Makonda Amkaa Kamanda Sirro....Adai anakula Rushwa za Wauza Shisha, Waziri Mkuu Atishia Kumtumbua Jipu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya
dawa za kulevya, aina ya shisha.
Hatua
hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega
kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu
waliotaka kumhonga lakini akakataa.
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa
Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam.
Wednesday, 16 November 2016
Dr. Shein Atia Saini Sheria ya Gesi na Mafuta.....Asema Wanaoikosoa Hawana Nia Njema na Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amesaini sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ya Zanzibar.
Mbali ya kusaini sheria hiyo, amewapiga kijembe wanaoikosoa sheria hiyo kuwa ni wachoyo na wasioitakia mema Zanzibar.
Dk.
Shein aliwaambia viongozi na waandishi wa habari kuwa sheria hiyo namba
6 ya mwaka 2016, inaipa Zanzibar mamlaka ya kisheria ya kuendeleza
rasilimali ya mafuta na gesi asilia.
Alisema kitendo cha kutia saini sheria hiyo, hakijavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama baadhi ya watu wanavyodai.
“Hakuna
aliyevunja sheria, anayevunja sheria wala atakayevunja sheria. Lakini
kama wao wanadai kutia saini sheria hii ni kuvunja sheria, basi watafute
suluhisho la kisheria,” alisema.
Aliwashauri
wenye mawazo hayo wakasome vizuri Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015
iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo
imeweka msingi imara wa kisheria wa kutambua rasilimali ya mafuta na
gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyoorodheshwa kwenye Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yanahitaji usimamizi bora na
imara wa kisheria.
Alisema
sheria hiyo imeainisha mambo makuu matatu ambayo kwanza ni kuwa
shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Bara
zitasimamiwa na taasisi zilizoanzishwa ndani ya sheria namba 21 ya 2015.
Sheria
hiyo inatamka pia kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa
upande wa Tanzania Zanzibar zitafanywa na taasisi zitakazoanzishwa kwa
mujibu wa sheria za Tanzania Zanzibar.
Kuhusu
mapato yatokanayo na shughuli hizo, Dk. Shein alisema sheria inatamka
upande wa Tanzania Bara mapato yatatumiwa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa faida ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa
Tanzania Zanzibar yatatumiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
faida ya Zanzibar.
“Kila
upande ulishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tulishauriana kwa
kina viongozi na tukapata ushauri wa kutosha kutoka kwa wanasheria wetu
wakuu hadi kufika bungeni,” alisema Dk. Shein.
Alisema
anatambua sheria hiyo ni mpya na anaelewa changamoto ambazo zinaweza
kutokea, lakini akatoa wito kwa wananchi kuiunga mkono na kushirikiana
na Serikali.
“Mafuta ni jambo kubwa katika maendeleo, pia yasipotumika vyema yanaweza kuitikisa nchi,” alisema Dk. Shein.
Aliwatahadharisha wananchi kutegemea mafanikio ya haraka kutoka sekta hiyo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla
iliyofanyika jana ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali
mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na
Ikulu.]
Viongozi
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya
utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa jana na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa
katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji
wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja jana
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na
Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika
hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa
Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Unguja jana.
RAIS KABILA HATOWANIA TENA URAIS KATIKA UCHAGUZI UJAO
Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao.
“Kwa wale ambao
wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema asante
lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi
inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa
mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya
wakongomani” Alisema Kabila.
Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.
Source: BBC
JOKATE,ABDU KIBA NA WENGINEO KUANZA KUACHIA KAZI CHINI YA LABEL YA ALI KIBA ' KING,S MUSIC'
Alikiba
amewataja wasanii ambao wapo chini ya lebo yake ya King's Music
wakiwemo Jokate, Abdu Kiba, Delila, Abby Skills na Brown Mauzo wa Kenya
kuwa ni baadhi ya wasanii ambao wapo chini ya label yake ambayo ameedai
ipo tangu siku yingi lakini hakuitangaza tu.“Mimi
Record label ninayo muda mrefu,muda mrefu sana lakini sikufanya
matangazo lakini nina wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika,
sasa hivi nimerudi tena najipanga upya nao waendelee kufanya kazi, kama
ambavyo unamuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea
kufanya kazi, pia kuna Abdu Kiba” Alikiba alifunguka kwenye 255 ya
Clouds Fm.
“Afu
vilevile kuna msanii mwingine ambao watu hawajawahi kumsikia, Pia kuna
wakiana Jokate, kina dalila na wengine wengi wapo chini ya label yangu,
sijafanya rasmi lakini mtawasikia
Subscribe to:
Posts (Atom)




















