Edward
Lowassa bado angali vinywani mwa wabunge japokuwa hayupo tena Bungeni
.Jina lake jana limeibua mjadala bungeni wakati wabunge walipotoleana
maneno makali kuhusu waziri huyo mkuu wa zamani.
Sakata
hilo limetokea wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipokuwa
likijadili Muswada wa Huduma ya Habari ambao ulipitishwa jana licha ya
kupingwa vikali na kambi ya upinzani na wadau wa habari.
Lowassa
amelizua tafrani bungeni baada ya wabunge wawili kurushiana maneno
kuhusu taarifa zake tofauti zilizokuwa zikiandikwa na vyombo vya habari
kiasi cha kusababisha mwenyekiti wa Bunge aingilie kati.
Akichangia
muswada huo, mbunge wa viti maalumu (CCM), Amina Mollel amerejea sakata
la zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond
Development ya Marekani ambayo ilibainika baadaye kuwa haikuwa na uwezo.
Sakata hilo lilitokea wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu.
“Mimi naomba ninukuu baadhi ya vichwa vya habari ambavyo vilitumiwa katika magazeti,” amesema Mollel, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.
Mollel ametaja mfano wa gazeti lililoandika “Lowassa anajua uzalendo au ni machozi ya mamba” na kichwa kingine cha habari cha gazeti hilo kilichosema “Lowassa Hasafishiki” na kingine kilichosema “Lowassa karibu Chadema”.
“Kuna
haja ya kuwa na waandishi ambao leo hii wanaandika habari kwamba mtu
huyo ni mbaya lakini kesho hiyo hiyo uongo huo unabadilika na kuwa
ukweli?”amehoji Mollel.
Amesema
Taifa linahitaji kuwa na sheria kama hiyo ambayo inaweza kulinda
taaluma ya waandishi wa habari, hivyo kupitishwa muswada huo ni kwa
manufaa ya wanahabari.
Maneno
hayo kuhusu Lowassa yakamfanya mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji
kusimama na kutumia methali inayosema “ukienda kwa wenye chongo, ufumbe
macho ili ufanane nao japokuwa unaona”.
“Leo
kituko cha karne hii ni pale anaponyanyuka mbunge wa CCM ndani ya Bunge
akatulaumu eti sisi (wabunge wa kambi ya upinzani) kwa sababu
tunampenda Lowassa. Hiki ni kituko cha karne,” amesema.
“Rudini kwenye kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa CCM kuhusu kale kawimbo katamu. Kweli?” amesema na kufanya wabunge wengine wa upinzani kuanza na kuimba “tuna imani na Lowassa”.
Jina
la Lowassa limekuwa likiibuka kwenye vikao mbalimbali na katikati ya
mwaka lilikuwa gumzo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ulioitishwa kwa
ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho,
No comments:
Post a Comment