Tuesday, 22 November 2016

Waliohamishiwa UDOM kutoka St Joseph kurudia mwaka

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Imewataka wanafunzi wa St. Joseph walioamishiwa katika chuo kikuu cha Dodoma kurudia mwaka kwa kile kilichobainika kuwa na ujuzi na maarifa usiokidhi viwango vya chuo cha Dodoma.

Wizara hiyo pia imesema kwamba watakaogomea uamuzi huo watatakiwa kurudi makwao .

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema, ni lazima wanafunzi hao warudie mwaka kwani wamepimwa na kubainika kuwa na uwezo mdogo hivyo hatua ya kuwataka kurudia mwaka ni nafasi ya pili kwao.

Prof. Ndalichako alisema, kwa sasa wizara yake inaandaa ripoti ya vyuo vinavyofundisha chini ya viwango ambapo amesema mara tu baada ya kukamilika ripoti hiyo, itatolewa na kwamba kwa wale wanafunzi ambao vyuo vyao vimefungwa kwa kutokidhi vigezo ni lazima wapimwe kiubora ili kupata wanafunzi watakao kidhi vigezo vya soko la ajira.

Aidha, Prof. Ndalichako ametoa onyo kwa wanafunzi ambao wamegushi nyaraka mbalimbali ikiwemo za vifo vya wazazi wao ama ugonjwa na kufanikiwa kupata mkopo wa elimu ya juu kwa njia ya udanganyifu kuwa wizara hiyo inafanya uhakiki na pindi watakapo bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Godbless Lema Kujaribu Tena Bahati yake Leo Mahakamani baada ya Kusota Mahabusu kwa Siku 19

Jaribio jingine la maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema linafanyika leo baada ya kusota mahabusu tangu akamatwe mkoani Dodoma Novemba 3. 
Lema anayekabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ombi hilo la dhamana linakuwa la tatu baada ya kukwama mara mbili tangu alipoingizwa mahabusu. 
Lema ambaye anatetewa na mawakili sita; Peter Kibatala, John Mallya, Charles Adiel, Adam Jabir, Faraja Mangula na Sheck Mfinanga, dhamana yake licha ya kutolewa na Hakimu Mkazi, Desdery Kamugisha ilipingwa kutokana na notisi ya rufani iliyowasilishwa na mawakili wa Serikali.

Baada ya notisi hiyo, Lema aliandika barua Mahakama Kuu kuomba mapitio ya kesi hiyo kwa maelezo kuwa taratibu za kisheria zilikiukwa kutokana na hakimu kutoa dhamana lakini akashindwa kukamilisha masharti ya dhamana na kupokea hoja za Jamhuri.

Hata hivyo, wakili mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi jingine kupinga Mahakama Kuu kufanya marejeo ya kesi hiyo.

Kadushi aliwasilisha hoja mbili za kisheria juu ya kuweka pingamizi la ombi la mbunge huyo kuwa muombaji hakukidhi vigezo vya kuiomba mahakama irejee  maamuzi ya mahakama kwa kuwa badala ya kuiandikia mahakama barua ya kuomba ifanye mapitio ya maamuzi hayo, angetakiwa akate rufaa juu ya maamuzi ya mahakama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 22

Monday, 21 November 2016

MAKONDA AITAKA TAKUKURU KUCHUNGUZA MADAI YA UFISADI MRADI WA AVIC TOWN

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amenusa ufisadi katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Avic ‘Avic Town’ na kuitaka taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuuchunguza mradi huo uliopo Kigamboni jijini humo.makonda-new-jpg-ooHatua hiyo imefika baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo na kutolewa pasipo kupewa fidia zao huku ekari 18 za Chama cha Mapinduzi (CCM),zikichukuliwa kwa matumizi katika mradi huo.
Akizungumzia hatua hiyo, Makonda amewataka watendaji wa serikali wanaohusika na taarifa za mradi huo kutoa taarifa sahihi katika vyombo vya dola kwani hataki kuona wananchi wakidhulumiwa haki zao.“Sitaki kuona kigogo wala kijiti anahusika katika mradi huo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Novemba 21

Rais Magufuli ateua Naibu Kamishna Mkuu wa TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 20 Novemba, 2016 amemteua Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Charles E. Kichere anajaza nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA iliyokuwa wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uteuzi huu umeanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Friday, 18 November 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 18

Mamlaka ya Bandari Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
 Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo. 
Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi. 

Wito Wa Kujiunga Na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria Na Vijana Kujitolea

Godbless Lema Akwama Tena Kupata Dhamana.......Arudishwa Gereza la Kisongo, Hatima Yake Kujulikana Wiki Ijayo


Hatma ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ilishindwa kujulikana jana baada ya mawakili wa Serikali kuweka pingamizi, wakipinga Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kusikiliza maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa mshtakiwa.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jaji Sekela Moshi, alisema   kutokana na pingamizi hiyo, atasikiliza hoja za sheria zilizowasilishwa mahakamani hapo kabla hajatoa uamuzi wowote juu ya dhamana ya mshtakiwa.

Aliwaelekeza mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za sheria kabla mahakama haijaendelea na hatua yoyote.

Jaji Moshi alisema atatoa uamuzi kuhusu mvutano huo wa sheria,  Novemba 22, mwaka huu

Wakuu 7 wa Mikoa Hatarini Kutumbuliwa kwa Kushindwa Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli

Wakuu wa mikoa saba wako hatarini kutumbuliwa kutokana na kushindwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati katika mikoa yao. 
Akizungumza jana alipokuwa akipokea madawati 3,500 yenye thamani ya milioni  300  kutoka benki ya NMB, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene alisema mikoa ya wakuu hao saba inaoongoza kwa upungufu wa madawati. 
Aliwataja kuwa ni wa Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma. 

Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli.

Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro, amesema kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua zaidi kwa sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani Dar es salaam.

Thursday, 17 November 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS NOV 17,2016

NIDA kuanza kutoa namba za utambulisho Desemba

Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia Desemba mwaka huu mpaka Januari 2017 itaanza kutoa namba maalum za utambuzi kwa wananchi.

Mkakati huo umetangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.

Alisema tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35 zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa zinazowahusu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.

Makonda Amkaa Kamanda Sirro....Adai anakula Rushwa za Wauza Shisha, Waziri Mkuu Atishia Kumtumbua Jipu

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha.

Hatua hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga lakini akakataa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam.

Wednesday, 16 November 2016

Dr. Shein Atia Saini Sheria ya Gesi na Mafuta.....Asema Wanaoikosoa Hawana Nia Njema na Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amesaini sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ya Zanzibar.

Mbali ya kusaini sheria hiyo, amewapiga kijembe wanaoikosoa sheria hiyo kuwa ni wachoyo na wasioitakia mema Zanzibar.

Dk. Shein aliwaambia viongozi na waandishi wa habari kuwa sheria hiyo namba 6 ya mwaka 2016, inaipa Zanzibar mamlaka ya kisheria ya kuendeleza rasilimali ya mafuta na gesi asilia.

Alisema kitendo cha kutia saini sheria hiyo, hakijavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hakuna aliyevunja sheria, anayevunja sheria wala atakayevunja sheria. Lakini kama wao wanadai kutia saini sheria hii ni kuvunja sheria, basi watafute suluhisho la kisheria,” alisema.

Aliwashauri wenye mawazo hayo wakasome vizuri Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo imeweka msingi imara wa kisheria wa kutambua rasilimali ya mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyoorodheshwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yanahitaji usimamizi bora na imara wa kisheria.

Alisema sheria hiyo imeainisha mambo makuu matatu ambayo kwanza ni kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Bara zitasimamiwa na taasisi zilizoanzishwa ndani ya sheria namba 21 ya 2015.

Sheria hiyo inatamka pia kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Zanzibar zitafanywa na taasisi zitakazoanzishwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania Zanzibar.

Kuhusu mapato yatokanayo na shughuli hizo, Dk. Shein alisema sheria inatamka upande wa Tanzania Bara mapato yatatumiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa faida ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa Tanzania Zanzibar yatatumiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa faida ya Zanzibar.

“Kila upande ulishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tulishauriana kwa kina viongozi na tukapata ushauri wa kutosha kutoka kwa wanasheria wetu wakuu hadi kufika bungeni,” alisema Dk. Shein.

Alisema anatambua sheria hiyo ni mpya na anaelewa changamoto ambazo zinaweza kutokea, lakini akatoa wito kwa wananchi kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali.

“Mafuta ni jambo kubwa katika maendeleo, pia yasipotumika vyema yanaweza kuitikisa nchi,” alisema Dk. Shein.

Aliwatahadharisha wananchi kutegemea mafanikio ya haraka kutoka sekta hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika jana ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.]
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana.

RAIS KABILA HATOWANIA TENA URAIS KATIKA UCHAGUZI UJAO



Photo: Joseph Kabila Kabange (R), President of the Democratic Republic of the Congo, during a meeting with German Foreign Minister Frank-Walter Steinmeier (not pictured), in Kinshasa, 19 February 2015. EPA/MICHAEL KAPPELER
Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao.
Akilihutubia bunge la taifa, Kabila ameomba kuwepo amani na utulivu.
“Kwa wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya
wakongomani” Alisema Kabila.
Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.

Source: BBC

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 16

JOKATE,ABDU KIBA NA WENGINEO KUANZA KUACHIA KAZI CHINI YA LABEL YA ALI KIBA ' KING,S MUSIC'


Alikiba amewataja wasanii ambao wapo chini ya lebo yake ya King's Music wakiwemo Jokate, Abdu Kiba, Delila, Abby Skills na Brown Mauzo wa Kenya kuwa ni baadhi ya wasanii ambao wapo chini ya label yake ambayo ameedai ipo tangu siku yingi lakini hakuitangaza tu.“Mimi Record label ninayo muda mrefu,muda mrefu sana lakini sikufanya matangazo lakini nina wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi nimerudi tena najipanga upya nao waendelee kufanya kazi, kama ambavyo unamuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi, pia kuna Abdu Kiba” Alikiba alifunguka kwenye 255 ya Clouds Fm.
“Afu vilevile kuna msanii mwingine ambao watu hawajawahi kumsikia, Pia kuna wakiana Jokate, kina dalila na wengine wengi wapo chini ya label yangu, sijafanya rasmi lakini mtawasikia

ALICHOKISEMA RAPPA TI BAADA YA TRUMP KUSHINDA URAIS

Baada ya Hillary Clinton kushindwa katika
uchaguzi mkuu nchini Marekani dhidi ya Donald Trump kumekuwa na mambo mengi sana yakiendelea.
 
TI na Donald Trump
Wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na
uchaguzi huo, huku wengine wakionesha kuwa tofauti na matokeo hayo.
Rapa T.I kwa upande wake alimpa pole rais
ambaye ana maliza muda wake, Barack Obama, kwa mteja wake kushindwa katika uchaguzi huo.
“Pole kwa matokeo ambayo kuna baadhi ya watu hawakuyatarajia, lakini tunafurahi tulikuwa na wewe kwa kipindi chote, lakini sasa tunasubiri kinachofuata,” alisema T.I.
Sasa Rapa wa ATL mtu mzima TI, amewataka wapenzi wa muziki wanao msapoti Rais Mteule Donald Trump kuacha kununua nyimbo zake.
TI ameuambia mtandao wa kidaku TMZ kuwa,
haoni faida ya kuwa na mashabiki wanao sapoti Sera za kibaguzi.
“Acha niseme tu kama una msapoti Donald Trump usijihusishe na muziki wangu, wapeni habari.” aliiambia TMZ.

Lowassa aeleza kwanini hakuhudhuria misiba ya Samwel Sitta na Mungai

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoonekana kwenye misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai.

Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki Mungai.

Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa.

Tuesday, 15 November 2016

Madini ya Bilioni 3 Yakamatwa Yakitoroshwa


Siku chache baada ya Rais John Magufuli kusema kuna utoroshaji mkubwa wa madini kupitia viwanja vya ndege vilivyopo migodini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umekamata madini yenye thamani ya Sh3,353,421,381.4 yakitoroshwa katika viwanja vikubwa vya ndege na katika matukio 25 tofauti.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMAA, Mhandisi Dominic Rwekaza ameeleza hayo katika ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na wakala huo mwaka 2015 akisema: “Katika kufuatilia usafirishaji wa madini nje ya nchi katika viwanja vikubwa tulikamata madini yanayotoroshwa yenye thamani ya Dola za Marekani 1,512,186.61 na mengine ya Sh34,670,794 katika matukio 25 tofauti.” 

TB Joshua avunja ukimya kuhusu utabiri wake kuwa Clinton angeshinda Urais


Siku kadhaa baada ya utabiri wa TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani kuwa tofauti, hatimaye mhubiri huyo maarufu wa Nigeria ametoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea.

Awali, TB Joshua aliwaambia waumini wake kuwa aliona ndotoni kuwa Rais wa Marekani atakayechaguliwa atakuwa mwanamke na kwamba atakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo jaribio la kutaka kumuondoa madarakani kwa kura za kutokuwa na imani naye.

Monday, 14 November 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Novemba 14

ACT-Wazalendo walaani kauli ya Serikali kutowajengea wananchi......Wadai kauli hiyo ni fedheha kwa waathirika na Wadau.

Watanzania wanakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera.

Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi. Jumla ya Watu 117,721 wameathirika kwa kupoteza makazi yao, mali na athari za kisaikolojia katika Wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba, Karagwe na Kyerwa.

Aidha, jumla ya watu 17 walipoteza maisha na 560 walijeruhiwa. Vilevile, nyumba 2,072 za makazi zilianguka kabisa na nyumba 14,595 za makazi zilibomoka, baadhi zina kuta au kupata nyufa kubwa na hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu. Vilevile, maafa haya yalisababisha uharibifu mbalimbali wa miundombinu ya barabara na majengo ya watu na taasisi mbalimbali, ikiwemo shule na Hospitali.

LEO NI LEO:HATIMA YA GODBLESS LEMA KUJULIKANA LEO ARUSHA

Wakati Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema (40) akitarajia kujua hatima ya dhamana yake katika Mahakama Kuu leo, kesho yeye na mkewe Neema Lema (33) watapanda kizimbani kwa kesi ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ijumaa iliyopita Lema alipelekwa Gereza la Kisongo, Arusha baada ya kunyimwa dhamana katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS ) amtaka Rais Shein asisaini muswada wa mafuta na gesi

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS ), Omar Said Shaaban amemshauri Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein asiusaini Muswada wa sheria ya mafuta na gesi uliopitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hivi karibuni kwa madai kuwa unavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Omari ameeleza msimamo huo katika barua yake ya maneno 1,293 aliyomwandikia Dk Shein akifafanua jinsi gani muswada huo unavunja sheria na Rais huyo anavyoingizwa kwenye mtego wa kuvunja Katiba.

Katika barua hiyo, mwanasheria hiyo anasema, “Mheshimiwa Rais, zipo taarifa kuwa unajiandaa kuweka saini kwenye muswada huo uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi ili hatimaye iwe sheria. Naomba nikunasihi uachane na mpango huo ili kujiepusha na mtego wa jaribio la kuvunja Katiba.”

Anasisitiza, “Kwa heshima naomba nikueleze kuwa jaribio la Serikali yako na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na hatua yako ya kuweka saini muswada huo ili uwe sheria, ni uvunjaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo wewe umeapa kuilinda, lakini pia ni kinyume na maelekezo ya sheria inayorejewa kama ndiyo chanzo cha mamlaka ya Zanzibar kutunga sheria yake.”

DONALD TRUMP AWEKA MGOMO KULIPWA MSHAHARA WA URAIS

Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani.

Trump ameweka msimamo huo jana katika mahojiano maalum na mtangazaji maarufu, Lesley Stahl katika kipindi cha 60 Minutes, aliyetaka kufahamu kuhusu uamuzi wake juu ya mshahara wake akiwa ni mfanyabiashara mkubwa.

Sunday, 13 November 2016

Friday, 11 November 2016

Picha: Rais Magufuli Alivyoongoza wananchi wa Dar kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 10 Novemba, 2016 aliwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Waziri na mbunge Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph James Mungai katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Picha: Rais Magufuli Alipomtembelea na Kumjulia Hali Mke wake na Wagonjwa wengine Waliolazwa Muhimbili

Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli, Janeth, amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Jana  Ikulu imetoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji.

Taarifa ya ikulu ilisema , alipokuwa anamjulia hali mkewe, pamoja na  balozi na waziri mstaafu wa Tanzania Omar Ramadhan Mapuri, wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji walimshukuru kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili

Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Yakamilisha Rasmi Taratibu Za Ajira Za Uhamiaji Kwa Ngazi Ya Askari Na Maafisa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Novemba 11

BARACK OBAMA NA FAMILIA YAKE KUHAMIA KWENYE MJENGO HUU



Baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi katika kura za Uraisi nchini Marekani, hebu pata nafasi ya kutazama mjengo ambao atakwenda kuishi Barack Obama akishatoka White House.

TANZIA: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia Alfajiri ya Leo Akiwa Mjini Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, Job Ndugai (Mb) anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Hafidh Ali Tahir amefariki dunia leo saa 9 alfajiri katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na Wabunge katika vikao  mpaka saa 2.45 usiku.

Serikali Yaanza Ujenzi Wa Reli Ya Kati.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) Bw.Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali imeanza Ujenzi wa reli ya kati,ujenzi wa kiwango cha Standard Gauge yenye upana wa Mita 1.345.
 
Akizungumza jana Jijini Dar es salaam na Waandishi wa Habari,Kadogosa alisema kuwa ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kwanza katika nchi ya Tanzania hasa baada ya Uhuru utapelekea kuleta na kuhamasisha maendeleo kwa haraka katika sekta ya Kilimo,biashara,Madini na viwanda.

Hata Hivyo Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa mradi wa Reli ya kati utaleta manufaa mengi ya kiuchumi na ya kijamii na kusaidia kuboresha pamoja na kuunganisha usafirishaji kwa nchi zisizokuwa na bandari kuelekea masoko ya Afrika na Dunia kwa ujumla.

"Kukamilika kwa Reli ya kati Utavutia uwekezaji katika maeneo ambayo mfumo huo wa Reli utapita na utaboresha usafirishaji,lakini pia utachochea maendeleo ya shughuli za Madini na usafirishaji wa nidhaa nje ya nchi, utasaidia kuokoa barabara zetu na kupunguza gharama kubwa ya ukarabati wa barabara,"alisema Kadogosa.

Pia aliongeza kuwa miradi hii imekuwa ikigharamiwa na Serikali ilikutimiza azma yake kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa ajili ya jamii ya watanzania hasa tunapoelekea katika uchumi wa viwanda kupitia sekta ya usafirishaji.

Thursday, 10 November 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Novemba 10

Wanafunzi hewa 65,198 wabainika shule za msingi, sekondari nchini

Jumla  ya wanafunzi hewa 65,198 wamegundulika kuwepo katika shule za msingi na sekondari nchini, ambako idadi ya wanafunzi hao isingebainika kiasi cha Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema kati ya wanafunzi hao wa shule za msingi ni 52,783 na sekondari ni 12,415.

Simbachawene alisema kazi ya uhakiki wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ilifanyika mikoa yote nchini kutokana na agizo la Ofisi ya Rais, Tamisemi kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Alisema waliagizwa kuhakiki idadi ya wanafunzi katika shule zote za msingi na sekondari kwa kulinganisha taarifa ilivyokuwa Machi mwaka huu wakati wa ujazaji wa madodoso ya takwimu za shule za awali, takwimu za shule za msingi, sekondari na nyaraka za mahudhurio ya wanafunzi.

Alieleza kuwa taarifa za idadi ya wanafunzi kabla ya kuhakiki Machi 2016, zilionesha kulikuwa na wanafunzi 9,746,534 wa shule za msingi na wanafunzi 1,483,872 wa shule za sekondari.

“Baada ya uhakiki tuliofanya Septemba mwaka huu, inaonesha kuwepo wanafunzi 9,690,038 wa shule za msingi na wanafunzi 1,429,314 wa shule za sekondari,” alieleza na kuongeza kuwa uchambuzi umeonesha kuwa wanafunzi 52,783 wa shule za msingi na wanafunzi 12,415 wa sekondari hawakutolewa maelezo ya uwepo wao shuleni.

Alisema kwa tafsiri rahisi hao ni wanafunzi hewa kwa shule za msingi na sekondari nchini, ambao idadi hiyo ya wanafunzi hewa kama isingebainika kwenye uhakiki huo na kupelekwa fedha, Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema kati ya fedha hizo Sh milioni 527.8 ni kwa shule za msingi na Sh milioni 403.4 ni kwa shule za sekondari.

Aliitaja mikoa inayoongoza kuwa na wanafunzi hewa ni Tabora (12,112), Ruvuma (7,743), Mwanza (7,349), Dar es Salaam (4,096), Kagera (4,763), Rukwa (4,054), Singida (3,239), Kilimanjaro (2,594), Kigoma (2,323), Njombe (2,307), Simiyu (2,081) na Arusha (1,923).

Mikoa mingine ni Mara (1,855), Tanga (1,378), Geita (1,281), Morogoro (1,172), Mtwara (882), Mbeya (786), Shinyanga (695), Songwe (512), Manyara (330), Dodoma (284), Lindi (281), Pwani (187), Iringa (161) na Katavi (0).

Waziri huyo alisema wanafunzi hewa walianza wakati serikali ilipoanza kupeleka fedha shuleni kama ruzuku.

Alisema Sh bilioni 27 zimekuwa zikipelekwa kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa shule na walimu wakuu, lakini baadhi ya walimu waliamua kuongeza idadi ya wanafunzi ili wapate fedha zaidi.

“Huu ujinga unaweza kufanywa hata katika ngazi ya wizara ni jambo la uchunguzi, zile fedha hazipiti Tamisemi zinakwenda moja kwa moja shuleni,” alieleza na kuongeza kuwa hatua za kinidhamu zinaendelea kuchukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa na Tamisemi inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa.

“Serikali haitegemei tena kuwepo suala la wanafunzi hewa. Naagiza makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa shule kuhakikisha suala la wanafunzi hewa halijitokezi tena katika shule zote za msingi na sekondari,” alibainisha Simbachawene.

Joseph Mungai Kuwagwa Leo Dar..........Mwili wa Samwel Sitta Kuwasili Leo

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa   Dar es Salaam leo katika viwanja vya Karimjee.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mtoto wa marehemu, William Mungai alisema ibada ya kuuaga mwili huo itafanyika katika viwanja hivyo saa 5.00 asubuhi.